Rasmi Antoine Semenyo amesaini mkataba wa kuitumikia Manchester City akitokea klabu ya AFC Bournemouth ya pale pale England.
Semenyo anakuwa mchezaji wa nne ghali wa Afrika kwenye ligi kuu ya England baada ya kununuliwa kwa kiasi cha Euro Milioni 72.
WACHEZAJI GHALI WA KIAFRIKA KWENYE LIGI YA ENGLAND (EPL)
N. Pepe Euro Milioni 80
B. Mbeumo Euro Milioni 75
O. Marmoush Euro Milioni 75
A. Semenyo Euro Milioni 72
R. Mahrez Euro Milioni 67.5
Semenyo raia wa Ghana amesaini mkataba wa miaka mitano na nusu na atavaa Jezi namba 42 ambayo aliwahi kuivaa nyota mwingine wa kiafrika Yayah Toure.
#manchestercity #transfer #transfernews