Tangu miaka ya 1980 Taifa stars imekuwa ikipambana kupata mafanikio makubwa kimataifa.
Ambapo tatizo si wachezaji kukosa kipaji,bali ni mfumo mzima wa soka nchini kuwa na changamoto.
Matatizo makuu:
1: Ukosefu wa uwekezaji wa kutosha.
* Nchi kama Morocco na South Africa zimewekeza kwenye viwanja vya kisasa,academy na sayansi ya michezo.
* mfano,Morocco ilianzisha akademi ya mohamed VI football Academy na sasa inazalisha wachezaji wa kimataifa kama Hakim Ziyech.
2:Ligi ya ndani kutokuwa imara vya kutosha.
* Ligi imara huzalisha timu ya taifa imara.
* mfano: Egypt inaligi yenye ushindani na uwekezaji matokeo yake Taifa lao limetwaa AFCON mara 7.
3: Academy chache na kukosa mfumo wa kuibua vipaji mapema.
* Nchi kama Senegal limefanikiwa kupitia Academy za mpira.
* Mfano: Generation football Academy ilimzalisha Sadio Mane,aliyekuwa nyota wa Liverpool na Bayern.
4.Maandalizi hafifu kabla ya mashindano .
* Timu nyingi za Afrika magharibi huanza kambi miezi kadhaa kabla ya mashindano.
* Mfano: Senegal hucheza mechi nyingi za kirafiki dhidi ya timu kubwa kama Brazil na Algeria kabla ya mashindano.
5: Kukosa mwendelezo wa sera na mipango.
* Kila kocha au uongozi ukija huanza upya badala ya kuendeleza alipoishia mwenzake.
Nini kifanyike ?(Suluhisho).
1: Uwekezaji kwenye miundo mbinu.
* Kujenga Academy za soka kila kanda kama ilivyofanya Senegal na Morocco.
2:Kuboresha ligi ya ndani.
* Kuongeza udhamini,usimamizi,na kutumia teknolojia(VAR,data analysis).
3: Kuanzisha mpango wa taifa wa kuendeleza vipaji.
* Vipaji viibuliwe mashuleni kuanzia umri wa miaka 12 hadi 17.
4. Kuongeza mechi za kimataifa za kirafiki.
* Mfano kucheza na timu bora ili kuongeza uzoefu.
* mfano:Japan iliboresha soka lake kwa kucheza na Brazil ,German na ufaransa mara kwa mara kabla ya kuwa na mafanikio.
5:Kutumia sayansi ya michezo.
*Fitness ,psychology,nutrition,performance analysis.
6:Kuwa na sera ya muda mrefu (10 to 15 years plan).
* Isibadilike kwa kubadilika kwa kocha au viongozi.
Taifa stars haijakwama kwa kukosa vipaji,bali kwa mfumo usiowezesha vipaji kustawi.
Tukiboresha Academy, ligi , maandalizi na uwekezaji tunaweza kuona mafanikio kama ya Morocco, Senegal na Egypt.
Na: Mbeki Mbeki.
Kagera.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime