Ndoa ni taasisi ya kijamii na kiroho inayounganisha mwanaume na mwanamke katika muungano rasmi na wakudumu.
Ingawa tamaduni na sheria hutofautiana kati ya jamii moja na nyingine ,Biblia huiweka ndoa katika kiwango cha juu zaidi,agano lililoanzishwa na Mungu mwenyewe.
Katika simulizi la uumbaji Mungu aliona si vema mwanadamu awe peke yake ,hivyo akamuumba mwanamke awe msaidizi anayemfaa ( mwanzo 2: 18_24).
Na hapa tunaona msingi wa kwanza wa ndoa.
Haikutokana na wazo la binadamu bali ni mpango wa Mungu.
Muungano huu unaelezwa kwa kauli nzito " Wawili watakuwa mwili mmoja"ikimaanisha umoja wa kiroho, kihisia na kimwili umoja unaopita urafiki wa kawaida.
Yesu kristo alirejea andiko hilo na kusisitiza kudumu kwa ndoa akisema " Alichounganisha Mungu ,mwanadamu asikitenganishe" (mathayo 19:5_6).
Hii inadhibitisha sifa yapili: ndoa si uhusiano wa muda bali ni muungano wa kudumu ,uliokusudiwa kudumu mpaka kifo.
Zaidi ya Muungano ndoa katika Biblia ni agano la uaminifu linalomhusisha pia Mungu kama shahidi na mlinzi wa ahadi hiyo( Malaika 2: 14).
Hivyo kuvunja ndoa si kosa la kijamii pekee bali ni jeraha la kiroho dhidi ya agano takatifu.
Biblia pia inatoa mwongozo wa wajibu ndani ya ndoa.
Mume anatakiwa kumpenda mke kwa upendo wa kujitoa,kama kristo alivyo lipenda kanisa( wefeso 5:25) na mke anatakiwa kumuheshimu mume( waefeso 5: 33).
Hii inaonyesha kuwa ndoa si mamlaka ya upande mmoja bali ni ushirika unaojengwa kwa upendo wa heshima.
Kwa ujumla ndoa kibiblia hubeba sifa kuu nne mpango wa Mungu,umoja,kudumu,na agano la uaminifu,likiongozwa na upendo wa kujitoa na heshima.
Changamoto za ndoa zinaweza kutikisa safari lakini haziwezi kufuta kusudi lake la msingi kuishi pamoja kwa ushirika,kusaidiana na kujenga familia katika maadili ya kimungu.
Aidha ndoa katika Biblia si sherehe wala cheti ,bali ni muungano wa agano unaobeba Saini ya Mungu ,wajibu wa upendo ,na wito wa kudumu.
Na: Mbeki Mbeki.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime