Tiger Woods amekataa kuiongoza timu ya Marekani Ryder Cup 2027 ili kuzingatia afya yake, baada ya ajali ya gari na tuhuma za kuendesha akiwa amelewa.
Nyota wa gofu Tiger Woods amekataa kuwa nahodha wa timu ya Marekani katika mashindano ya Ryder Cup ya mwaka 2027.
Chama cha PGA cha Amerika kimesema Woods amechukua uamuzi huo ili kuzingatia afya yake na ustawi wa muda mrefu.
Hatua hiyo inakuja baada ya Woods kushtakiwa kwa kuendesha gari akiwa amelewa kufuatia ajali ya barabarani wiki iliyopita, ingawa hakupata majeraha.
Polisi waliripoti dalili za ulevi na walipata dawa aina ya hydrocodone ndani ya gari lake, ambayo hutumika kutibu maumivu makali.
Woods, mshindi wa mataji makubwa 15, alikuwa akitarajiwa kuiongoza timu ya Marekani katika mashindano hayo yatakayofanyika Ireland, lakini sasa hatakuwepo kutokana na changamoto zake za kiafya.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime