Taifa Stars yashuka nafasi ya ubora FIFA

Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imeshuka kwa nafasi tatu katika viwango vya ubora wa soka duniani vinavyotolewa na FIFA, na sasa kushika nafasi ya 113 kutoka 110 iliyokuwa nayo mwezi Februari.

Kuporomoka huko kunahusishwa na kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Liechtenstein National Team katika mashindano ya FIFA Series 2026, ambapo wapinzani hao walikuwa katika nafasi ya 205 kabla ya mchezo huo.

Kwa upande wa ukanda wa Afrika Mashariki, Kenya imepanda hadi nafasi ya 112, huku Uganda ikisalia nafasi ya 88 na Rwanda ikipanda hadi nafasi ya 129.

Katika nchi za CECAFA, South Sudan imeonyesha mafanikio makubwa kwa kupanda hadi nafasi ya 164 Kimataifa, Spain inaendelea kuongoza, ikifuatiwa na France huku Argentina ikishika nafasi ya tatu.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii