Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetoa adhabu kwa mchezaji wa klabu ya Young Africans SC Djigui Diarra kufuatia ukiukwaji wa kanuni za ligi.
Adhabu hiyo inahusiana na tukio lililotokea katika mechi namba 126 ya Ligi Kuu ya NBC kati ya Mtibwa Sugar FC dhidi ya Young Africans SC iliyomalizika kwa sare ya mabao 1-1 katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya TPLB Djigui Diarra amefungiwa michezo mitatu (3) Pia ametozwa faini ya shilingi 2,000,000 (milioni mbili) kwa kosa la kumshambulia mwamuzi wa kati baada ya kumalizika kwa mchezo huo.
Aidha mchezaji huyo ametozwa tena faini ya shilingi 2,000,000 (milioni mbili) kwa kosa la kuonesha ishara isiyofaa (kidole cha kati) wakati akitoka uwanjani.
Adhabu hizi zimetolewa kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu ya NBC hususan kifungu kinachohusu nidhamu ya wachezaji.
Hata hivyo TPLB imesisitiza kuwa vitendo vya utovu wa nidhamu havitavumiliwa na imezitaka klabu kuhakikisha wachezaji wao wanazingatia maadili na sheria za mchezo wa mpira wa miguu.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime