Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linamtafuta kijana mmoja (jina limehifadhiwa) kwa tuhuma za kumuua Abel Mganga Mazuri (25), mkazi wa Nyamahengo, na kuwajeruhi watu wawili.
Ingawa tukio hilo limetokea Machi 24, 2026 majira ya saa 5:30 usiku katika kitongoji cha Nyamahengo, kata ya Sumve.
Kamanda wa Polisi Mkoa, Wilbrod Mutafungwa, amesema shambulio hilo lilitokea wakati mtuhumiwa akiwa na wenzake wakinywa pombe na kuangalia mpira, ambapo ugomvi ulizuka kutokana na ushindani wa timu za Simba SC na Yanga SC.
Polisi wamesema mtuhumiwa alitumia kitu chenye ncha kali kushambulia watu watatu, na kusababisha kifo cha Abel Mazuri.
Aidha waliopata majeraha ni Semen Juma Cherehani (26) na Ndubu Mkoi Chagula (26), ambao sasa wapo katika Hospitali Teule ya Sumve wakipatiwa matibabu, huku hali zao zikikaribia kuimarika.
Hata hivyo jeshi la Polisi linaendelea na msako mkali kumtafuta mtuhumiwa, huku wakiwataka wananchi kuepuka vurugu zinazohusiana na ushabiki wa mpira ili kuhakikisha usalama unadumishwa.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime