Nyota wa Liverpool FC, Mohamed Salah, ametangaza rasmi kuondoka klabuni hapo kupitia ujumbe wa hisia aliowaandikia mashabiki, akieleza kuwa amefikia uamuzi wa kuanza safari mpya nje ya Anfield.
Katika ujumbe wake, Salah ameishukuru klabu, jiji na mashabiki kwa kuwa sehemu muhimu ya maisha yake, akisisitiza kuwa Liverpool si klabu tu bali ni historia na upendo wa kipekee.
Aidha amehitimisha kwa kuahidi kubeba kumbukumbu hizo milele huku akiendelea kuiheshimu kauli mbiu ya klabu ya “You’ll Never Walk Alone.”
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime