Mashabiki Ulaya walalamikia bei kubwa Tiketi za FIFA World Cup 2026

Mashabiki wa kandanda barani Ulaya wamewasilisha malalamiko rasmi kuhusu gharama kubwa ya tiketi za FIFA World Cup 2026 inayotarajiwa kufanyika Amerika Kaskazini.

Malalamiko hayo yamewasilishwa na Football Supporters Europe (FSE) kwa kushirikiana na Euroconsumers, kupitia waraka wa kurasa 18 uliowasilishwa kwa Halmashauri Kuu ya European Union mjini Brussels.

Aidha katika taarifa yao ya pamoja, mashirika hayo yamedai kuwa FIFA inatumia udhibiti wake katika mauzo ya tiketi kuweka masharti yasiyokubalika katika soko la ushindani, huku wakieleza kuwa bei za tiketi zimepanda kupita kiasi ukilinganisha na mashindano yaliyopita.

Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa hiyo, tiketi za fainali zitakazopigwa katika MetLife Stadium zinakadiriwa kuanzia dola 4,185, kiasi ambacho ni zaidi ya mara saba ya bei ya tiketi ya chini kabisa ya fainali ya Kombe la Dunia la mwaka 2022 iliyofanyika nchini Qatar.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii