Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu, anatarajiwa kuzungumza katika mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa unaoendelea jijini Washington nchini Marekani leo Alhamisi.
Hotuba yake inatarajiwa wakati huu akilenga kuchaguliwa tena kama Waziri Mkuu wa Israeli kwa muhula mwengine.
Mzozo wa Palestina unatarajiwa kutawala siku ya tatu ya mkutano huo wa UN, mkutano ambao hata hivyo Rais wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas hajahudhuria baada ya kunyimwa visa na Marekani.
Abbas atahutubia mkutano huo kupitia njia ya video kama ilivyokuwa kwa mwaka uliopita.
Wachambuzi wa masuala ya kiusalama wanasema huenda Netanyahu akautumia mkutano huo kuzikashifu nchi ambazo amekuwa akisema zinazuia Israeli kufanikisha malengo yake mashariki ya kati.
Suala la Iran pia litakuwa kwenye agenda yake, amekuwa akiituhumu Tehran kama nchi mfadhili wa makundi ya kigaidi mashariki ya kati likimwemo kundi la Hamas na Hezbollah, makundi anayosema ni ya kigaidi.
Benjamin Netanyahu pia amedai kuwa atasema ukweli kuhusu Meya wa New York, Zohran Mamdani, ambaye anamtuhumu kwa kuunga mkono kundi la Hamas.