karibia milipuko 20 ilisikika, jeshi la anga la Ukraine likitoa tahadhari kwa raia kuhusu makombora ya Urusi yaliokuwa yamerushwa kuelekea Kyiv.
"Mji umeshambuliwa kwa makombora. Ingieni katika maeneo salama!" Meya wa Kyiv Vitali Klitschko aliandika kwenye mtandao wa Telegram.
Mashambulio haya mapya yamejiri wakati Rais wa Ukraine akikutana na wabunge wa bunge la Marekani jijini Washington ambapo amewataka kuiwekea Urusi vikwazo zaidi.
Zelensky amesema Urusi imeendelea kushambulia Mji wa Kyiv, miundombinu ya kiraia, makazi ya watu, hospitali za kina mama wajawazito, miundombinu ya nishati na ile ya usafiri.
Mji wa Kyiv wenye idadi ya watu karibia Milioni tatu umeendelea kuripoti mashambulio ya Urusi, kila pande zikiripotiwa kutumia makombora ya masafa marefu kwenye mzozo huo.