WAHAMIAJI HARAMU ZAIDI YA 190 WAKAMATWA MKOANI DODOMA. ? ?

‎Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Dodoma imefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu zaidi ya 190 kutoka mataifa mbalimbali kwa kipindi cha septemba 2025 kufuatia Oparesheni Maalumu inayoendelea nchi nzima.

‎‎Hayo yamesemwa leo Septemba 29 mwaka huu Jijini Dodoma na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji SACI Dkt. Agness Luziga, Afisa Uhamiaji Mkoa wa Dodoma wakati akitoa taarifa fupi ya Oparesheni hiyo kufuatia kukamatwa kwa Wahamiaji haramu  37 waliokamatwa mwishoni mwa wiki iliyopita katika maeneo mbalimbali Mkoani Dodoma mara baada ya kufanya Oparesheni, Misako na doria ili kudhibiti Wahamiaji haramu nchini.

‎‎SACI Dkt. Luziga amesema Wahamiaji hao haramu tayari wamechukuliwa hatua mbali mbali ikiwemo kufikishwa mahakamani  na wengine kuondoshwa nchini.

‎‎Aidha ametoa Rai kwa Wananchi kuendelea kushirikiana na Idara ya Uhamiaji Kupitia Kampeni ya Mjue Jirani yako Ili kuendelea kuwabaini Wahamiaji haramu na hatimae kuwachukulia hatua za kisheria kwa manufaa ya kizazi cha sasa na baadae. 

‎‎Idara ya Uhamiaji Tanzania inaendelea na Operesheni Maalumu Nchi nzima kwa lengo la Kudhibiti wimbi la Wahamiaji haramu Ili kuimarisha Ulinzi na Usalama wa Taifa hususani katika kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii