Ujumbe wa Korea watembelea Soko la Bidhaa Tanzania

Ujumbe wa wafanyabiashara kutoka kampuni 15 za Jamhuri ya Korea ukiongozwa na Mwenyekiti wa Kampuni ya KOIMA Bi. Youn Young Mi umetembelea Soko la Bidhaa Tanzania (TMX) ili kuangazia ushirikiano wa kibiashara kwa kununua bidhaa za mazao za Tanzania. 

Akizungumza baada ya kukamilika kwa wasilisho lililoandaliwa na TMX kuelezea kazi za TMX na maeneo ya ushirikiano, Mkuu wa Idara ya Sheria na Katibu wa Bodi ya TMX, Bw. Selenga Kaduma amewakaribisha wafanyabiashara hao ili kuweza kuichagua TMX kama mfumo rasmi wa kununua bidhaa za mazao hapa nchini. 

Naye Bi. Youn ameeleza kuvutiwa na wasilisho la kina walilopata kutoka TMX kwani limegusia maeneo ambayo wangependa kujikita nayo zaidi katika ushirikiano baina yao na Tanzania.

TMX ni wauzaji wa mazao mbalimbali yakiwemo kokoa, dengu, mbaazi, soya na korosho.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii