RC Mtanda Aweka Msisitizo: Hakuna Kupandisha Bei Ramadhan na Kwaresma

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda, ametoa onyo kali kwa wafanyabiashara wa masoko mbalimbali mkoani humo dhidi ya tabia ya kuongeza bei za vyakula na bidhaa nyingine bila sababu za msingi kuelekea Mwezi Mtukufu wa Ramadhan na kipindi cha Kwaresma.

Akizungumza na baadhi ya wafanyabiashara pamoja na Maafisa Biashara wa Mkoa katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mtanda amesisitiza umuhimu wa kuzingatia uadilifu na maadili ya biashara, akiwataka kutochukua fursa ya msimu wa sherehe na ibada kuwaumiza wananchi kwa kupandisha gharama kiholela.

Ameeleza kuwa Serikali ya Mkoa haitasita kuchukua hatua kali kwa mfanyabiashara yeyote atakayebainika kukiuka taratibu na sheria za biashara, akibainisha kuwa vyombo vya dola vitashirikiana kwa karibu kusimamia hali ya soko.

“Hatutaruhusu mwananchi anyanyasike kwa kupandishiwa bei bila sababu halali. Wafanyabiashara wanapaswa kuzingatia sheria na misingi ya haki katika utoaji wa huduma,” amesisitiza Mtanda.

Ameongeza kuwa lengo la serikali ni kulinda maslahi ya wananchi na kuhakikisha upatikanaji wa bidhaa muhimu unaendelea kwa bei stahiki katika kipindi chote cha Ramadhan na Kwaresma.

Sasa ili kupata undani wa  taarifa hii tafadhali usikose kutufuatilie na Usikilize jembe Habari Kamili hapo saa moja  kamili jioni ambapo msomaji wetu wa hii leo ni Jacob Mlay tafadhali usipitwe na taarifa zetu Mahiri kabisa.

Lakini pia tembelea mitandao yetu ya kijamii ya Jembefmtz

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii